Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), safarini kuelekea Arusha, tarehe 21 Novemba, 2025, ambako anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, kesho tarehe 22 Novemba, 2025.